Wednesday, April 18, 2012

mei 19 washindi wa kill music award kugonga show sokoine mbeya


.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanaro Premium Lager ambao ni wadhamini wakuu wa Tuzo za Muziki Tanzania (KTMA) April 17 2012 wamezindua rasmi ziara ya washindi wa tuzo za Kili 2012 ambapo hiyo Tour itafanyika katika mikoa 6 ya Tanzânia na kuhusisha uvumbuzi wa vipaji vichanga vya wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya, Mtwara na kilele kuwa Dar es Salaam.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro George Kavishe amesema “tutawapa nafasi wasaniii watakaovumbuliwa kuimba na washindi vinara wa tuzo za Kili ambapo mshindi mmoja wa kila mkoa ataletwa Dar es Salaam kushiriki kwenye tamasha la mwisho la ziara, na pia kurekodiwa nyimbo moja ya kumwezesha kuanza safari yake ya muziki.

.
Kati ya wasanii watakaoshiriki kwenye ziara hizo za washindi wa tuzo za Kili ni pamoja na Diamond, Khadija Kopa, Suma Lee, Warriours from the East, Ali Kiba, AT, Aisha Msharuzi, Twanga Pepeta, Ben Pol, Roma, Ommy Dimples, Kalijo Kitokololo, Jaguar na Barnaba.

Ziara za tamasha zitaanzia Dodoma tarehe 28 Aprili (Jamuhuri Stadium), – Mwanza tarehe 5 Mei (CCM Kirumba), Kilimanjaro tarehe 12 Mei(Ushirika Stadium), Mbeya tarehe 19 Mei (Sokoine Stadium), Mtwara tarehe 26 mei (Mtwara Stadium) na Dar es Salaam tarehe 2 June (leaders club).
Uvumbuzi wa vipaji utafanyika kwenye mikoa mitano kila mwisho wa juma, wiki moja kabla ya tarehe ya tamasha, ikianza na Dodoma tarehe 22 April (Club 84), Mwanza tarehe 29 April(Villa Park), Kilimanjaro tarehe 6 Mei (Mr. Price- Moshi), Mbeya tarehe 13 Mei (Vibes) na Mtwara tarehe 20 Mei (Maisha club) ambapo Majaji wa kuamua mchakato wa uvumbuzi wa vipaji ni pamoja na Juma Nature, Proffessor Jay na Queen Darleen.

No comments:

Post a Comment