Friday, December 21, 2012

DAKTARI WA RUFAA MBEYA ATIWA MBARONI KWA MADAI YA KUPOKEA RUSHWA

DAKTARI wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32), amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, akikabiliwa na mashitaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi 100,000 kutoka kwa mgonjwa aliyefikishwa Hospitalini hapo baada ya kupata ajali.


Hatua hiyo imekuja baada ya Taasisi ya kuzui na Kuipambana na rushwa nchini takukuru, kumtia mbaroni daktari huyo juzi kwa tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha baada ya kumuwekea mtego.
Daktari huyo Kisabi amepandishwa kizimbani  majira ya saa 3:45 na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Fransis Kishenyi, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo ambayo imeibua hisia kali kwa wananchi.
Katika kesi hiyo namba 237 ya mwaka 2012, upande wa mashitaka uliongozwa na waendesha mashita wawili wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU), Joseph Mulebya na Nimrod

No comments:

Post a Comment